Habibi

Nimependa banati mtulivu
Ila majibu yake naona wivu
Nimempenda kwa moyo wangu wote
Nikitakacho kwake ni tuwe sote
Kaajaliwa na urembo timilifu
Kiwa nami ntajihisi mkamilifu
Kimwana tano kwa tano
Kila akipita napata homa ya manjano
Ana asili ya waja wa Mlima Kenya
Nimwonapo nahisi kana kwamba moyo kaumenya
Ila kumwambia nasitasita
Nikihofia nafsi kupigwa vita
Nifanyeje na moyo wamuita???

Leave a comment

Design a site like this with WordPress.com
Get started