Ni wengi yamewaliza,
Wengine yamewaliwaza,
Yanacho kiza,
Yanao pia mwangaza,
Tamu kama pizza,
Katu mja huwezi mkataza,
Yana uchungu mate kumiza
Yana utamu wake, roho kufaza
Yana visasi,kulipiza
Kiungulia,hisia kukata ja mashaza
Akili sanasana kuwaza
Furaha moyoni kujaza
Yanayo taharuki ya giza
Mja hali kumchakaza
Hali yake kuwazawaza
Nafsi kufurahi,nafsi kukwaza
Ila sana hupendeza
Moyo kudekezaā¦
Nasisitiza
Ni wengi yamewaliza
Wengine yamewaliwaza

Leave a comment