Una urembo kama hurlaini wa peponi
Hisia zangu wazitia motoni
Kila usiku u mwangu ndotoni.
Macho yako mazuri
Umbo lako nane namba
Unanukia uturi
Una Sauti kama kasuku
Na nyodo kama vifungo
Ni mwenye hakika huba
Mahaba moyoni yamenikaba
Penzi moto zaidi ya jua
Wewe umeniridhi wengine wote pangua
Napenda ulivyo, mso maringo
Mahaba ndo langu kuu lengo
Nakupenda, dhambi kusema uongo