La azizi nakupa yangu yamini
Huba langu ni lile lile la yakini
Umenizidi moyoni na mwangu akilini
Wanivisha tabasamu daima mdomoni
Najawa na furaha iliyozidi pomoni
Njoo nikudekeze mwangu kifuani
Visokoro kwinyo wanyongwe kooni
Nimekupenda mpaka ndani rohoni
Mwengine sitamani kuwa naye maishani
KJ 📖✍🏾🇰🇪

Leave a reply to Mimi Ndiye 🇰🇪 Cancel reply