Tag: Mapenzi

  • Hidaya

    La azizi nakupa yangu yamini
    Huba langu ni lile lile la yakini
    Umenizidi moyoni na mwangu akilini
    Wanivisha tabasamu daima mdomoni
    Najawa na furaha iliyozidi pomoni
    Njoo nikudekeze mwangu kifuani
    Visokoro kwinyo wanyongwe kooni
    Nimekupenda mpaka ndani rohoni
    Mwengine sitamani kuwa naye maishani

    KJ πŸ“–βœπŸΎπŸ‡°πŸ‡ͺ

  • Beda

    Ninajua mchakato unauma
    Ila ndio hujenga ushuhuda
    Kwa hivyo sina budi
    Ila kukubaliana na hali
    Nikijua kuna ushindi
    Mwisho wa safari
    Maana MUNGU wangu si tapeli
    Sina mashaka na Yeye
    Bado Namwamini

  • Mahbuba

    I never told them about you
    But they saw you in my written words
    The perfume of love cannot be concealed

Design a site like this with WordPress.com
Get started