Sikujaliwa na moyo wa chuma
Kuhimili yako mahaba na maumivu
Kanichoma, mtima waniuma
Tele, roho yangu imejaa maumivu
Maisha yamenikwisha yake hamu
Kanitia karaha moyoni mwangu
Usoni mwangu sinayo tena tabasamu
Nashindwa kukuita tena mpenzi wangu
Tazamio langu nilidhani tatizo marafiki
Wachochezi wenye hulka za kinafiki
Kumbe yote ni wewe, kunguru na mwewe
Asali nilipenda, kaona heri kuchonga mzinga
Hakika nyuki kumfuga sharti ukubali na kuumwa
Maumivu chungu nzima nashindwa kuvumilia
Hisia mfarakano, moyoni nalia
Penhive βπΎ




